Kaduna

mji mkuu wa jimbo la Kaduna nchini Nigeria From Wikipedia, the free encyclopedia

Kadunamap
Remove ads

Kaduna ni mji mkuu wa jimbo la Kaduna kaskazini-kati mwa Nigeria. Mji huo, ambao uko kwenye Mto wa Kaduna, ni kiini cha biashara kubwa na usafiri kwa maeneo ya kilimo yaliyo karibu pamoja na reli na makutano ya barabara.

Ukweli wa haraka Country, State ...
Thumb
Mto Kaduna.

Idadi ya wakazi wa Kaduna ni 8,252,400.

Ishara ya Kaduna ni mamba, aitwaye Kada katika lugha ya Kihausa .

Remove ads

Historia

Kaduna ilianzishwa na Waingereza mwaka wa 1913 na kuwa mji mkuu wa Nigeria wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini mwaka 1917. [1] Ilihifadhi hali hiyo mpaka 1967.

Watu waliotoka Kaduna ni pamoja na Emmanuel na Celestine Babayaro (wachezaji mpira wa Nigeria) na Fiona Atlanta (mwanasinema wa Uingereza na msichana katika sinema ya Bond)

Ugomvi wa Kidini

Kaduna imekuwa mahala pa mvutano wa kidini kati ya Waislamu na Wakristo, hasa juu ya utekelezaji wa sheria katika shari'a katika mji wa Kaduna mwanzo wa mwaka wa 2001. Hasa katika tukio moja Februari mwaka wa 2000 angalau watu 1,000 waliuawa katika zogo fulani. Mji unabakia umetengwa siku hizi, ambapo Waislamu hasa wanaishi kaskazini mwa mji na Wakristo kusini. [2] Tukio jingine lilitokana na makala katika gazeti Lagos ambayo yalitia Waislamu hasira. Makala ilikuwa juu ya shindano la kutafuta Mrembo wa Dunia lililokuwa wiki hiyo katika mji mkuu wa Abuja, kupendekeza kwamba kama Muhammad angehudhuria shindano hilo angeweza kuoa mmoja wa washindani hao. [3]

Remove ads

Elimu

Kaduna ni nyumbani mwa Chuo cha Ulinzi cha Nigeria (1964), Kaduna Polytechnic (1968), Chui kikuu cha Ahmadu Bello (1962), Chuo kikuu cha Kaduna(2007), Chuo cha Urobani na Teknolojia cha Nigeria na Taasisi ya Utafiti wa Trypanosomiasis Nigeria (1951).

Uchumi na usafiri

Kaduna ni kituo cha viwanda Kaskazini mwa Nigeria, vinatengeneza bidhaa kama nguo, mashine, chuma, alumini, bidhaa za mafuta na magurudumu.

Ufinyaji wa Udongolinalofanywa sana katika Kaduna, hasa kutoka Maraban-Jos, ambayo inayofuata Abuja na Minna. Njia kuu inayopiytia mji huu inaitwa Barabara Ahmadu Bello. Majina mengi ya maeneo katika mji huu yametokana na majina ya zamani Masultani, emirs na mashujaa wa vita. Kaduna ina soko kubwa,lilioundwa hivi karibuni baada ya moto katikati mwa mwaka wa 1990.

Kuna uwanja wa mashindano mkubwa, takriban maili moja mviringo, ambapo ndani mnaKlabu ya polo ya Ahmadu Yakubuna Kalabu ya mamba Kadunapia vilabu vya mchezo wa raga viko ndani mwa uwanja huo. Kuna viwanja vya ndege mbili, moja ambayo ni Uwanja wa ndege Kaduna .

Ofisi kuu ya Kampuni ya huduma za ndege ya Chanchangiiko Kaduna. [4]

Njia za reli

Mnamo Septemba, mwaka wa 2009, ujenzi wa tawi la reli hadi mji mkuu wa Abuja ulipitishwa [5]

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads