Kanisa la Wakaldayo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kanisa Katoliki la Wakaldayo (kwa Kiaramu ܥܕܬܐ ܟܠܕܝܬܐ ܩܬܘܠܝܩܝܬܐ , ʿītha kaldetha qāthuliqetha) ni mojawapo kati ya Makanisa Katoliki ya Mashariki, likifuata mapokeo ya Mesopotamia na kutumia liturujia ya Mesopotamia[1].

Idadi ya waamini leo ni zaidi ya 600,000[2] [3], wengi wao wakiwa wenyeji wa Mesopotamia.
Remove ads
Historia
Kanisa hilo linachanga historia moja na Kanisa la Asiria hasa hadi mwaka 1552, lilipotokea farakano kati yao, huku waliojiita Wakaldayo wakiungana na Kanisa Katoliki kama walivyotangulia kufanya wenzao kadhaa wa Cyprus mwaka 1445[4]
Muundo
Kanisa hilo linaongozwa na Patriarki wa Baghdad, Iraki, kwa sasa Louis Raphaël I Sako (kwa Kisiria: ܠܘܝܣ ܪܘܦܐܝܠ ܩܕܡܝܐ ܣܟܘ) aliyezaliwa tarehe 4 Julai 1948 na anayeishi Baghdad.[5]
Chini yake kuna majimbo katika nchi hiyo (250,000 waamini), katika nchi nyingine za Mashariki ya Kati (Iran, Siria, Uturuki, Lebanon na Misri) na kwenye mtawanyiko uliotokana na waamini kuhama kwa sababu ya hali ngumu hasa ya vita na dhuluma: Marekani, Kanada, Australia na New Zealand n.k.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads