Kupro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kupromap
Remove ads

Kupro, rasmi kama Jamhuri ya Kupro, ni kisiwa kilichoko katika Bahari ya Mediterania, mashariki mwa Ugiriki na kusini mwa Uturuki. Inapakana kwa karibu na nchi kama Syria, Lebanon, Israel, na Misri kupitia bahari. Kupro ina idadi ya watu takriban milioni 1.2, na ni miongoni mwa nchi ndogo kwa ukubwa wa idadi ya watu barani Ulaya. Mji wake mkuu na jiji kubwa zaidi ni Nicosia. Nchi hii imegawanyika katika sehemu mbili kuu – eneo la Kusini linalotawaliwa na Jamhuri ya Kupro na eneo la Kaskazini linalojitawala na kujulikana kama Jamhuri ya Kupro ya Kaskazini, ambayo inatambuliwa rasmi na Uturuki pekee. Kupro ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2004.

Ukweli wa haraka
Remove ads


Thumb
Ramani ya Kupro
Remove ads

Historia

Kisiwa cha shaba

Watu waliishi huko walau kuanzia milenia ya 10 KK.

Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo cha shaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki. Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa hicho.

Katika Biblia

Kisiwa kinazungumziwa na Biblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana na umisionari wa Mtume Barnaba na wenzie Mtume Paulo na Marko Mwinjili kisiwani huko.

Karne za Kati

Kuanzia mwaka 649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa na Waarabu walioua wakazi wengi na kubomoa makanisa na miji mizima.

Chini ya Waosmani

Baada ya Wakristo kujirudishia kisiwa hicho muhimu, Waturuki Waosmani walikiteka mwaka 1570 na kuingiza Uislamu bila kufaulu kufuta dini ya awali.

Chini ya Waingereza

Mwaka 1878 Uingereza ulianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi na Dola la Waosmani hadi mwaka 1914.

Uhuru

Tarehe 16 Agosti 1960 Kupro ilijipatia uhuru ingawa kulikuwa na utata kati ya kubaki peke yake, kuungana na Ugiriki au kugawiwa kati ya kaskazini (Waturuki) na kusini (Wagiriki).

Baada ya uhuru

Tangu vita vya Kupro, 1974 kisiwa kimegawiwa, huku maeneo ya kaskazini yakiwa yanatawaliwa na Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa.

Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004.

Remove ads

Watu

Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kigiriki, wengine Kituruki, ambazo zote mbili ni lugha rasmi.

Kwa jumla hao wa kwanza ni Wakristo (72.3% za wakazi wote), wa pili ni Waislamu (25%).

Wakristo karibu wote ni Waorthodoksi; wengine ni Wakatoliki (2.9%, hasa Wamaroni), Waprotestanti (2%) na Waarmenia.

Dini ina nafasi kubwa katika maisha ya wananchi.

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Government
Tourism
Official publications

35°N 33°E

Maelezo zaidi Nchi za Umoja wa Ulaya ...
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads