Karachi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Karachi
Remove ads

Karachi (Kiurdu: كراچى) ni mji mkubwa wa Pakistan na mji mkuu wa jimbo la Sindh. Hadi 1959 ilikuwa mji mkuu wa kitaifa. Mji ni kitovu cha kibiashara cha Pakistan.

Ukweli wa haraka Habari za kimsingi, Mahali ...

Karachi iko kando la delta ya mto Indus mwambaoni wa Bahari Arabu. Kuna mabandari mawili na viwanda vingi.

Mohammed Ali Jinnah anayekumbukwa kama baba wa taifa la Pakistan alizaliwa pia kuzikwa mjini.

Remove ads

Historia

Eneo la Karachi lilikaliwa na watu tangu muda mrefu na miji mbalimbali ya kihistoria imeaminiwa kuwepo katika eneo lake tangu zamani za Aleksander Mashuhuri aliyepita hapa. Katika karne ya 17 palikuwa na kijiji cha wavuwi kilichoitwa "Kolachi". Kikakua kuwa bandari ya biashara na Bara Arabu. Baada ya kuungwa kwa Sindh katika Uhindi wa Kiingereza mnamo 1843 Waingereza waliona nafasi nzuri ya bandari hiyo wakaanza kupanga na kukuza mji. 1864 mawasiliano ya simu ilianzishwa kati ya Karachi na London. 1878 mji ukaunganishwa na reli za Uhindi. Mwisho wa karne ya 19 idadi ya wakazi ilipita lakhi moja.

Wakati wa utengano wa Uhindi wa Kiingereza nusu ya wakazi walikuwa Wahindu waliopaswa kukimbia Uhindi. Wakimbizi Waislamu kutoka Uhindi walichukua nafasi yao wako sasa takriban nusu ya wakazi wote wa mji.

Baada ya Uhuru wa Pakistan Karachi ilikuwa mji mkuu hadi 1959.


Remove ads

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads