Kasio wa Narni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kasio wa Narni (alifariki Narni, Italia ya Kati[1], 29 Juni 558 BK) anakumbukwa kama askofu wa mji huo kuanzia mwaka 536 hadi kifo chake[1].
Aliwahi kuoa Fausta lakini baadaye alimuacha aishi kitawa[2]. Alikuwa maarufu kwa upendo wake kwa maskini hata akasifiwa na Papa Gregori I, anayesimulia alivyomtolea Mungu kila siku sadaka ya upatanisho kwa kumwaga machozi mengi na alivyokuwa anatoa kwa wahitaji kila alichokuwanacho. Hatimaye, siku ya kuadhimisha sherehe ya Mitume Petro na Paulo, ambayo alizoea kwenda kila mwaka huko Roma, kisha kuadhimisha Misa na kuwapatia wote Mwili wa Kristo katika mji wake, alirudi kwa Bwana.[3].[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads