Keremkerem

From Wikipedia, the free encyclopedia

Keremkerem
Remove ads
Remove ads

Keremkerem ni ndege wa familia ya Meropidae. Wana mwili mwembamba wa rangi maridadi. Mdomo wao ni mrefu na mwembamba na mkia wa aina nyingi za keremkerem una mileli mirefu katikati.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Ndege hao wanaishi uwandani kwa kanda ya tropiki na nusu-tropiki ya Afrika, Ulaya na Asia. Hula wadudu, nyuki, manyigu na mabunzi hasa, ambao wanakamatwa hewani. Kabla ya kula, ndege anatoa mshale wa mdudu akimgongea tawi la mti au kitu kigumu kingine.

Keremkerem hupenda kuwa pamoja kwa makundi. Huchimba mashimo ndani ya kando za mchanga kwa kutaga mayai yao meupe.

Familia ya Meropidae imegawika katika nusufamilia mbili: Nyctyornithinae (keremkerem wenye ndevu) na Meropinae (keremkerem wa kawaida).

Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Spishi za Asia

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads