Kokoko-mlasamaki

Ndege mbuai wa familia Strigidae From Wikipedia, the free encyclopedia

Kokoko-mlasamaki
Remove ads

Kokoko-walasamaki ni ndege mbuai wa jenasi Ketupa na Scotopelia katika familia Strigidae. Siku hizi wataalamu wengi wanawaainisha katika jenasi Bubo. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na wana mnasaba na kungwi.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Ndege hawa wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe pamoja na madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi za Ketupa zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio.

Kokoko-walasamaki wanatokea karibu na mito na maziwa katika misitu minene. Huwinda usiku na hula samaki hasa lakini amfibia na wanyama wadogo pia.

Jike huyataga mayai 1 au 2 lakini mara nyingi kinda moja aishi tu. Kwa kawaida tago lao ni kwenye mti mkubwa lakini katika shimo la mwamba pia.

Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads