Kungwi (ndege)

Ndege mbuai wakubwa wa familia Strigidae From Wikipedia, the free encyclopedia

Kungwi (ndege)
Remove ads

Kungwi ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Striginae katika familia Strigidae. Spishi fulani zinaitwa kokoko. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na spishi za jenasi Bubo ni miongoni mwa spishi kubwa kabisa za Strigidae.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Kungwi wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe pamoja na madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi nyingi zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio

Ndege hawa hula mamalia wadogo na wakubwa kiasi hasa (mpaka paa mdogo) lakini ndege, watambaazi na wadudu pia. Kokoko-walasamaki hula samaki hasa. Huwinda usiku.

Kwa kawaida jike huyataga mayai 2 lakini 1-5 inawezekana. Tago lao ni ardhini, mitini, kwenye miamba iliyojitokeza nje na hata kwenye vishubaka vya madirisha.

Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Spishi za mabara mengine

Remove ads

Spishi za kabla ya historia

  • Bubo binagadensis (Mwisho wa Pleistocene ya Binagady, Azerbaijan)
  • Bubo florianae (Mwisho wa Miocene}
  • Bubo leakeyae (Mwanzo wa Pleistocene ya Tanzania)
  • Bubo osvaldoi Cuban Horned Owl, (Mwisho wa Pleistocene ya Kuba)
  • Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Senèze, Ufaransa)
  • Bubo sp. (Mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewskie, Polandi)
  • Bubo sp. (Mwisho wa Pleistocene ya San Josecito Cavern, Mexiko)
  • Pulsatrix arredondoi (Mwisho wa Pleistocene ya Cueva de Paredones, Kuba)

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads