Mfalme Arthur

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mfalme Arthur
Remove ads

Mfalme Arthur ni mhusika mashuhuri katika masimulizi ya mitholojia ya Britania. Anakumbukwa kama mfalme aliyeishi katika kasri yake ya Camelot akiwa na upanga wake unaojulikana kama Excalibur, aliopewa na Bibi wa Ziwa (the Lady of the Lake).

Thumb
Sanamu ya Mfalme Arthur kwenye kanisa la Hofkirche, Innsbruck, iliyoundwa na Albrecht Dürer na kukalibiwa na Peter Vischer Mzee, mnamo miaka ya 1520

Katika kumbukumbu hiyo Arthur alikuwa kiongozi au mtawala wa Britania katika kipindi ambako Waroma walikuwa wameondoka tayari na Waanglia-Saksoni walivamia kisiwa na kuenea humo.

Kufuatana na masimulizi hayo Arthur alifaulu kuwashinda mara kadhaa. Hadithi moja maarufu ya Mfalme Arthur ni ile ambapo anatoa upanga kutoka kwa jiwe, tendo linalomfanya kuwa Mfalme wa Wabritania.

Hakuna uhakika kama Arthur aliishi kweli; labda masimulizi juu yake ni kumbukumbu ya kiongozi fulani wa Britania aliyeitwa jina tofauti[1].

Remove ads

Camelot

Kuna kasri mbalimbali zinazodaiwa kuwa ni Camelot ya Arthur, lakini ile inayokubaliwa na wengi zaidi ni kasri ya Tintagel, Cornwall (ingawa hakuna ushahidi). Huko Camelot Artur alikaa kwenye meza ya mviringo (the round table), pamoja na malkia wake Guinevere, Merlin, Morgan le Fay, Sir Lancelot, Sir Gawain, Percival na mashujaa wengine. Arthur na mashujaa wake waliondoka huko kwenda safari kama ile ya kutafuta Kikombe cha Kristo (Holy Grail).

Remove ads

Kifo

Baada ya vituko vingi mtoto wake, Mordred, alinyakua ufalme wake pamoja na malkia. Hivyo alimlazimisha Arthur kupigana naye. Walipigana kwa muda mrefu na Mordred alimpiga King Arthur katika sehemu nyingi, lakini mwishowe ni Arthur aliyemuua Mordred. Baada ya ushindi huo, Mfalme Arthur alikuwa dhaifu akafa kutokana na kupoteza damu kutoka kwa majeraha yaliyopatikana katika mapigano. Wakati mashujaa wake walipokuwa wakirudi Camelot, walitupa upanga Excalibur ndani ya ziwa ili uweze kurudi ulikotokea. [2] Hadithi moja ni kwamba Arthur hakuwahi kufa lakini atarudi wakati Waingereza watakuwa wanamhitaji.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads