Masiya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.[1]



Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu[2]
Hata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli[3] katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani[4]
Remove ads
Katika Ukristo
Jina hilo lilitafsiriwa na Septuaginta kwa Kigiriki Χριστός (Khristós)[5] nalo lilitumiwa mapema na Wakristo wa lugha hiyo kwa Yesu wa Nazareth kwa sababu ya kusadiki ndiye mkombozi aliyetimiza kikamilifu kila utabiri wa manabii wa Agano la Kale. Ndiyo sababu jina lake la awali limekuwa linaongezewa kwa kawaida hilo la Kristo, hivi kwamba imezoeleka kumuita Yesu Kristo.
Kwa asili ni tamko la imani lenye sehemu mbili: jina "Yesu" na cheo "Kristo".
Katika lugha ya Kigiriki "Yesu Kristo" mara nyingi ni sentensi kamili, maana yake "Yesu ndiye Masiya wa Mungu", yaani Yesu ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale na kutazamiwa na Israeli.
Katika aya nyingine za Agano Jipya "Yesu Kristo" tayari imetumika kama jina (linganisha: rais Mkapa, au: Mkapa rais - si yule Mkapa mwingine...)
Kutokana na umuhimu wa imani hiyo kwa wafuasi wa Yesu[6], wenyewe walianza kuitwa Wakristo huko Antiokia, mji wa kwanza kuwa na waumini wenye asili ya kimataifa na waliozungumza Kigiriki kuliko wale wenye asili ya Kiyahudi. Kumbe katika mazingira ya Kisemiti wanaendelea kuitwa kama awali Manasara, yaani Wanazareti.
Remove ads
Katika Uislamu
Hadithi za Uislamu pia zinafundisha kwamba nabii Isa, mwana wa Bikira Mariamu, alikuwa ametabiriwa kama Masih (المسيح) wa Waisraeli, na kwamba atarudi duniani siku ya Kiyama, pamoja na Mahdi, ili kumsinda Masih ad-Dajjal, yaani Mpingakristo.[7]
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads