Kipini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kipini
Remove ads

Kipini ni kijiji cha wavuvi kwenye pwani ya Kenya katika Kaunti ya Tana River. Iko kilomita 20 kusini mwa Witu kwenye mdomo wa Mto Tana unapoishia katika Bahari Hindi.

Thumb
Ramani ya Kipini kwenye mdomo wa Mto Tana.
Thumb
Mwambao wa Kipini.

Historia

Kipini imetambuliwa kuwa mji wa kihistoria ya Waswahili katika Kenya ya leo. [1] Kuna mabaki ya makaburi yaliyojengwa kwa mawe ambayo yanafikiriwa kuwa na asili katika karne ya 11[2].

Katika karne ya 19 Kipini ilitajwa katika mkataba baina ya Ujerumani na Uingereza kama mpaka wa kaskazini wa maeneo ya Sultani wa Zanzibar yaliyotambuliwa nao, mbali na Lamu na miji kadhaa.[3] Hivyo ilikuwa pia kwa muda mpaka wa kaskazini wa koloni la Kenya kwenye pwani[4].

Baadaye wakati wa ukoloni Kipini ilikuwa makao makuu ya wilaya ya Lower Tana.

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads