Kitabu cha Tobiti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kitabu cha Tobiti ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Nakala zilizopatikana katika mapango ya jumuia ya Waeseni huko Qumran zinaonyesha kuwa kitabu hicho kiliandikwa kwanza kwa Kiaramu miaka 200 KK hivi na kutafsiriwa mapema kwa Kigiriki katika Septuaginta.
Inaonekana kuwa tafsiri ya Kilatini maarufu kwa jina la Vulgata iliyofanywa na Jeromu inategemea andiko asili.
Kitabu hicho kilikubaliwa kama sehemu ya Biblia na mtaguso wa Hippo (393), mtaguso wa Carthago wa mwaka 397 na wa mwaka 419, halafu tena na Mtaguso wa Florence (1442) na Mtaguso wa Trento (1546)[1][2][3][4][5][6].
Lakini hakikubaliwi na Wayahudi katika Tanakh, wala na Waprotestanti wengi.
Hadithi hiyo inahusu familia ya kabila la Naftali la taifa la Israeli katika karne ya 7 KK, baada ya uhamisho uliosababishwa na Waashuru.
Lengo lake kuu ni kufundisha maadili bora ya Wayahudi
Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads