Kitakasa mikono

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kitakasa mikono
Remove ads

Kitakasa mikono (kwa Kiingereza: hand sanitizer) ni kiowevu au jeli inayotumika kupunguza pathojeni (viini viambukizavyo magonjwa) kwenye mikono.[1] Kitakasa mikono hugawiwa kwenye ngozi kwa kuchuana mikono. Kwa njia hiyo pathojeni zinazokaa kwenye ngozi ya mikono huuawa au kudhoofishwa kabisa. Ufanisi hutegemea aina ya dawa inayotumiwa ndani ya kitakasa na aina za pathojeni zinazolengwa, kama ni bakteria, virusi au fungi.

Thumb
Kitakasa mikono.

Aina nyingi za vitakasa mikono huwa na kiwango cha alikoholi kisichopungua asilimia 60. Ilhali alikoholi inasababisha ngozi kuwa kavu sana. mara nyingi dawa kama gliserini inaongezwa inayokinga ngozi.

Katika mazingira ya matibabu kitakasa mikono hupendelewa kuliko kunawa mikono kwa maji na sabuni. [2] [3]

Nje ya kliniki na hospitali kunawa mikono hupendelewa kwa ujumla.[4] [5]

Vitakasa kwenye msingi wa alikoholi kwa kawaida huwa na isopropanoli au ethanoli. Michanganyiko huwa na asilimia 60-95 za alikoholi. Tahadhari ni muhimu kwa sababu inaweza kuwaka.[2]

Vitakasa vya kialikoholi humaliza viini vingi lakini si spora.[6] Kuongeza gliserini hukinga dhidi ya kukauka kwa ngozi.

Shirika la Afya Duniani limetoa mwongozo wa kutengeneza kitakasa mikono kwa kutumia kemikali zinazopatikana karibu katika kila nchi. Kulingana na mwongozo huo, kutengeneza lita 10 za kitakasa mikono, zifuatazo zinachanganywa pamoja, na hutiwa maji yaliyochemshwa kwa lita 10[7]

Remove ads

Umuhimu wa kutakasa mikono

Mikono ni njia kuu ya kusambaza viini vya kuambukiza na hapa kuna umuhimu wa kutakasa mikono mara kwa mara katika mazingira yenye pathojeni.

Hii ilionyeshwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1846 ambapo tabibu Ignaz Semmelweis aliagiza wauguzi na madaktari katika hospitali yake ya Vienna kunawa mikono katika maji ya klorini kabla na baada ya kuwahudumia wagonjwa; alipunguza vifo kwa zaidi ya asilimia 90.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads