Vienna

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vienna
Remove ads

Vienna (kwa Kijerumani: Wien) ni mji mkuu na mji mkubwa wa Austria. Uko mashariki mwa nchi, kando ya mto Danubi.

Ukweli wa haraka Nchi, Jimbo ...
Thumb
Sehemu za Mji wa Vienna
Thumb
Vienna

Idadi ya wakazi imezidi milioni moja na laki tisa[1].

Vienna ina cheo cha jimbo ndani ya shirikisho la jamhuri ya Austria.

Remove ads

Utawala

Vienna imegawiwa katika mitaa 23.

  1. Innere Stadt (kitovu cha jiji)
  2. Leopoldstadt
  3. Landstraße
  4. Wieden
  5. Margareten
  6. Mariahilf
  7. Neubau
  8. Josefstadt
  9. Alsergrund
  10. Favoriten
  11. Simmering
  12. Meidling
  13. Wilaya ya 13
  14. Penzing
  15. Rudolfsheim-Fünfhaus
  16. Ottakring
  17. Hernals
  18. Währing
  19. Döbling
  20. Brigittenau
  21. Floridsdorf
  22. Donaustadt
  23. Liesing
Thumb

Utamaduni

Thumb
Kanisa Kuu la Mt. Stefano ni kati ya majengo mashuhuri ya Vienna
Thumb
Mnara wa Danubi Vienna
Thumb
Kisiwa la Danubi
Thumb
Mtaa wa Rotenthurm
Thumb
Kanisa la Vienna Christian Center, Sky Campus ndani za mnara ya Gasometer
Thumb
Maria-Theresia-Platz
Thumb
Ngome ya Schoenbrunn

Kwa karne nyingi Vienna ilikuwa mji mkuu wa dola kubwa. Wafalme na makaizari wa familia ya Habsburg walitawala Dola Takatifu la Kiroma hadi mwaka 1806 na baadaye na maeneo makubwa ya Ulaya ya kusini-mashariki hadi mwaka 1918. Hivyo Vienna ina majengo mazuri yanayotunza kumbukumbu ya enzi hizo, sio tu mji mkuu wa Austria ndogo ya leo.

Watu wa Vienna hukumbuka wasanii walioishi katika mji wao kama watunga muziki Wolfgang Amadeus Mozart, Ludwig van Beethoven na Johannes Brahms.

Remove ads

Mbuga na bustani

Thumb
Bustani ya mji Vienna
Thumb
Bustani ya ikulu ya "Schönbrunn" kwa mtazamo wa "Gloriette"

Bustani kadhaa za shirikisho la Austria ziko Vienna. Bustani maarufu zaidi ni Bustani ya Jumba la Schönbrunn, bustani nyingine ni "Augarten", "Belvedergarten", "Burggarten", "Volksgarten" na Bustani ya mji Vienna.

Sanaa na utamaduni

Thumb
Uchoraji katika kituo cha chini cha ardhi cha Volkstheater

Opera ya Serikali iko kwenye Karlsplatz.

Kuna majumba ya makumbusho mengi huko Vienna, pamoja na Bundesmuseum 'Albertina', historia ya sanaa na majumba ya makumbusho ya asili, majumba ya makumbusho ya sanaa iliyotumiwa na ya kisasa, "Belveder", jumba la makumbusho la kiufundi na maktaba ya kitaifa ya Austria.

Vituo vingine vya chini ya ardhi pia vimeundwa kisanii. Kwa mfano, kituo cha chini cha ardhi cha Volkstheater na kituo cha Aspern Nord kwenye uwanja wa Nelson Mandela.

Remove ads

Usafiri

Thumb
Mstari wa tram 60 ya Treni za barabarani Vienna huko "Westbahnhof"
Thumb
Ramani ya mtandao ya "U-Bahn", "S-Bahn", "Lokalbahn" na treni za mkoa huko Vienna, tarehe 2020

Kuna huduma za treni ya masafa marefu Railjet, Nightjet, Intercity, Westbahn na Intercity-Express.

Remove ads

Campsite

Kuna Campsite mbili Vienna, Campsite Vienna West / Wienerwald na Campsite Vienna Danube mpya.

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads