Kulturkampf

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kulturkampf
Remove ads

Kulturkampf (kwa Kijerumani "Vita vya utamaduni") ni jina la ushindani kati ya serikali za nchi kadhaa, hasa Dola la Ujerumani chini ya chansela Otto von Bismarck, na Kanisa Katoliki katika karne ya 19[1][2][3][4][5][6].

Thumb
Mwenye heri Papa Pius IX (1878 hivi).
Thumb
Chansela Otto von Bismarck (1875 hivi).

Serikali nyingi zilitaka kushika mamlaka zote juu ya raia zake, wakati Papa na maaskofu hawakupenda kupotewa na athira zao za muda mrefu juu ya waumini katika masuala ya kijamii.

Ushindani huo ulipata nguvu ya pekee Ujerumani baada ya nchi hiyo kuunganishwa chini ya Prussia na kutenga Austria. Hapo dola jipya lilijikuta kuwa na asilimia ya Waprotestanti kubwa kuliko awali ambapo Wakatoliki walikuwa wengiwengi. Hasa Prussia iliyoongoza dola hilo ilikuwa ya Kiprotestanti kabisa.

Mgongano ulisababisha serikali ya Prussia na ya Dola lote kutunga mfululizo sheria za kubana Kanisa Katoliki, na pia kufunga maaskofu wake.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads