Kwintiani wa Rodez

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kwintiani wa Rodez
Remove ads

Kwintiani (kwa Kilatini: Quintianus, Quinctianus; kwa Kifaransa: Quintien; alifariki 13 Novemba 525 au 526) alikuwa askofu wa Rodez, halafu, kwa kufukuzwa na Wagoti, wa Clermont-Ferrand (Arvernes) katika karne ya 6, na kwa msingi huo alishiriki Mtaguso wa Agde (508) na Mtaguso wa kwanza wa Orléans (511).

Thumb
Mt. Kwintiani katika dirisha la kioo cha rangi.

Kadiri ya Gregori wa Tours alizaliwa barani Afrika. Akiwa padri wa Karthago alikimbilia Ufaransa kutokana na dhuluma za Wavandali dhidi ya Wakatoliki[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2][3], lakini pia 14 Juni[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads