Shakwe

From Wikipedia, the free encyclopedia

Shakwe
Remove ads

Shakwe ni ndege wa familia Laridae. Watu wengi huita spishi za Sternidae shakwe pia. Spishi za Laridae zina michanganyiko ya rangi nyeupe, nyeusi na ya kijivu; nyingine ni nyeupe kabisa, nyingine kijivucheusi. Ndege hao wana domo lenye nguvu na ncha kali; domo lao ni nene kuliko lile la spishi za Sternidae. Wanaweza kuogelea na wana ngozi kati ya vidole vyao.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Shakwe huhusiswha na pwani, na kweli huko wako tele, lakini spishi nyingi wanatokea mbali na bahari, kwa kawaida karibu na maji. Spishi za Rissa huonekana baharini mbali na pwani. Shakwe huwakamata samaki wadogo au kaa au gegereka wengine lakini hula mizoga pia. Hulitengeneza tago lao chini, mara nyingi kisiwani.

Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Spishi za mabara mengine

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads