Lauryn Hill

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lauryn Hill
Remove ads

Lauryn Noel Hill (amezaliwa tar. 26 Mei 1975) ni mshindi mara nane wa Tuzo za Grammy akiwa kama mwimbaji, rapa, mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi za muziki, na mwigizaji bora wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Lauryn Hill. Katika shughuli zake za awali, alianza kujibebea sifa kubwa katika ulimwengu wa muziki wa hip hop akiwa kama mwanamke pekee wa kundi la muziki huo la The Fugees.

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Thumb
Lauryn Noel Hill (2019)

Mnamo 25 Agosti katika mwaka wa 1998, akaanza kufanya kazi kama msanii wa kujitegemea na kuweza kutoa albamu moja iliyompatia mafanikio makuwa kabisa. Albamu ilikwenda kwa jina la The Miseducation of Lauryn Hill, albamu iliyosaidia kuinua muziki wa neo-soul katika ngazi za kibiashara.

Baada ya miaka minne ya mapumziko, akatoa albamu ya MTV Unplugged No. 2.0 iliyorekodiwa mnamo 21 Julai 2001 katika studio za MTV. Hill ameshinda tuzo nane za Grammy na pia ni mama wa watoto watano aliozaa na Rohan Marley, mtoto wa nne wa mwanamuziki wa raggae wa zamani - Bob Marley.

Remove ads

Wasifu

Maisha ya awali

Lauryn Hill alizaliwa mnamo tar. 26 Mei ya mwaka wa 1975, katika mji wa East Orange, New Jersey. Hill alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa na mwalimu wa Kiingereza - Valerie Hill na mwekaji programu za kompyuta Mal Hill. Akiwa mtoto, Hill alikuwa akisiliza rekodi nyingi muziki wa soul uliokuwa unafanywa na wazazi wake na studio za Motown zile za miaka ya 1960.

Muziki huo ulikuwa karibu kidogo na nyumbani kwa kina Hill. Mal Hill alikuwa akiimba nyimbo katika maharusi, Valerie alikuwa akipiga piano, na kaka mkubwa wa Lauryn Melaney alikuwa akipiga saxophone, gitaa, ngoma, harmonica, zeze, na piano.

Hill alianza kazi za uimbaji wakiwa na umri mdogo sana. Mnamo mwaka 1988 akiwa na umri mwa miaka 13, Hill alianza kuonekana katika maonyesho ya usiku akiwa kama mwimbaji kujitolea wa katika maonyesho ya It's Showtime at the Apollo.[1][2][3]

Remove ads

Muziki

Albamu zake

Maelezo zaidi Maelezo ya albamu ...

Single zake

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Single alizoshirikishwa na baadhi ya vibwagizo

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Mwonekano wake katika nyimbo nyingine

  • 1996: "Stay Gold" (kutoka katikaYoung Zee albamu yaMusical Meltdown (Promo LP))
  • 1996: "If I Ruled the World" (kutoka katikaNas albamu yaIt Was Written)
  • 1997: "Retrospective For Life" (kutoka katikaCommon albamu yaOne Day It'll All Make Sense)
  • 1998: "On That Day" (kutoka katikaCeCe Winans albamu yaEverlasting Love)
  • 1998: "A Rose Is Still A Rose" (kutoka katikaAretha Franklin albamu yaA Rose Is Still a Rose)
  • 1999: "All That I Can Say" (kutoka katikaMary J. Blige albamu ya"Mary (album)"
  • 1999: "Turn Your Lights Down Low" kutoka katikaBob Marley tribute albamu yaChant Down Babylon)
  • 1999: "Do You Like The Way" (kutoka katika Carlos Santana albamu yaSupernatural)
  • 2002: "Selah" (from Divine Secrets of the Ya-Ya Sisterhood Soundtrack)
  • 2004: "The Passion" (from The Passion of the Christ: Songs)
  • 2005: "So High (Cloud 9 Remix) (kutoka katikaJohn Legend kutolewa kawa albamu ya"Get Lifted")
  • 2007: "Music" (kutoka katikaJoss Stone albamu yaIntroducing Joss Stone)
  • 2007: "Lose Myself" (kutoka katikaSurf's Up kibwagizo)
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads