Leodegari wa Autun

From Wikipedia, the free encyclopedia

Leodegari wa Autun
Remove ads

Leodegari wa Autun (kwa Kilatini: Leodegarius; kwa Kifaransa: Léger; Autun, Saône-et-Loire, 615 hivi – Sarcing, Somme, Picardie, 2 Oktoba 679) alikuwa askofu wa Autun, leo nchini Ufaransa, mtoto wa mtakatifu Sigrada [1][2].

Thumb
Kifodini cha Mt. Leger. Mchoro mdogo wa mwaka 1200 hivi unaonyesha alivyotobolewa macho.

Kwa kuwa alimpinga Ebroini, mkuu wa ikulu ya mfalme Theodoriki III, aliyetaka kupindua utawala wa ukoo wa Wamerovinji, aliteswa kikatili, akapofushwa akauawa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3]. Pamoja naye anaheshimiwa ndugu yake Warinus aliyeuawa na Ebroini miaka miwili kabla yake kwa kupigwa mawe [4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads