Leza

From Wikipedia, the free encyclopedia

Leza
Remove ads

Leza (kutoka Kiingereza laser, akronimi ya fungu la maneno "Light Amplification by Stimulated Emission of Radiation"[1][2]) ni chombo cha kukuza na kushadidisha miali kuelekea upande mmoja kutengeneza mwangaza leza.

Thumb
Leza Nyekundu(660 & 635 nm), kijani(532 & 520 nm) na bluu (445 & 405 nm)

Kifaa hiki ni maalumu, si kama taa nyingine za kutoa mwangaza na miali yake ina matumizi mengi.

Remove ads

Historia

Leza ina historia kubwa na ni mojawapo wa nyanja zilizofanyiwa utafiti mkubwa tangu mwaka 1917. Utafiti wa leza umekua kutokana na utafiti wa mnururisho (radiation) na utafiti wa usumakuumeme (electromagnetism).

Manufaa ya leza

Leza ina matumizi mengi yakiwemo:

  • Burudani - inatumika kwa vifaa vinavyosoma vijisahani rekodi (disc drives) na vifaa zinazotoa miali ya rangi tofautitofauti katika nyumba za burudani
  • Biashara kwa vifaa kama vile vya kupiga chapa, vya kupima joto vya leza, vielekezi leza na vinginevyo
  • Viwandani kutengeneza vifaa vya leza vya kukata, kuchomelea, kupima urefu kidijiti, kutia alama vitu na kuchomea vitu zinazoundwa kwa joto
  • Mawasiliano - kupeperusha mawimbi ya runinga na intaneti[1]
  • Usalama - katika ala za vita hasa tochi za kulenga shabaha katika vifaa vya kivita kama vile bunduki za kisasa, kuelekeza kombora za kisasa
  • Matibabu - kufanya operesheni isiyo ya upasuaji[3]
  • Upodozi - kufanya operesheni zisizo za upasuaji za kubadilisha umbile ili kuongeza urembo kama vile operesheni ya lipo ya leza (ijulikanayo kwa Kiingereza kama "Liposuction") inayopunguza mafuta mwilini. Operesheni ya lipo hufanywa na mashine ya lipo ya leza ambayo ilibatilisha mfumo wa zamani wa operesheni ya lipo ambao watu walifanyiwa upasuaji.
Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads