Lukungu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lukungu
Remove ads

Lukungu ni ndege wa familia Trogonidae. Wanatokea misituni kwa tropiki katika Afrika, Asia na Amerika. Ndege hawa wana ukubwa wa kwenzi mkubwa. Rangi zao ni kali na spishi za Afrika zina tumbo jekundu na mgongo kijani. Hula wadudu hasa lakini spishi za Amerika na Asia hula matunda pia. Dumu au dumu na jike pamoja huchimba tundu katika mti unaooza au kichuguu ili kutaga mayai ndani yake. “Violaceous trogon” hutengeneza tago lake mara nyingi ndani ya tundu la nyigu. Jike huyataga mayai 2-4. Makinda huota manyoya haraka sana: katika wiki mbili hadi tatu, pengine wiki nne.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads