Lumbila

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lumbila
Remove ads

Lumbila ni kata ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59406.

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Thumb
Mahali pa Lumbila kwenye Ziwa Nyasa

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 2,038 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 1,880 [2] walioishi humo.

Remove ads

Historia

Wakati wa kuanzishwa kwa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kituo cha Langenburg kilianzishwa hapa mwaka 1893 kando ya mdomo wa mto Luyangala (Wajerumani waliandika "Rumbira"). Langenburg ilikuwa makao makuu ya serikali kwa sehemu za kusini za koloni kwa sababu usafiri ulipatikana kwa njia ya maji tu, ilhali Wajerumani hawakusimamia bado njia za ndani hadi kukandamizwa kwa upinzani wa Wahehe mnamo mwaka 1898 (kifo cha Mkwawa).

Langenburg ilikuwa na boma imara na kituo cha meli ndogo "Hermann von Wissmann" yenye tani 50 iliyokuwa chombo kikuu cha usafiri cha Wajerumani kwenye Ziwa Nyasa na kuzunguka baina ya Langenburg, Wiedhafen (Manda), Fort Johnston (Mangoche, Malawi), Monkey Bay na vituo vingine upande wa Kiingereza wa ziwa.[3]

Mwanzoni Langenburg ilikuwa makao makuu ya Mkoa wa Langenburg lakini baadaye ofisi zilihamishwa katika eneo la Unyakyusa ambako mji mpya ya Neu Langenburg (leo: Tukuyu) ulianzishwa. Kwa kuitofautisha miji miwili jina la Alt-Langenburg ilikuwa kawaida kwa kituo cha kwanza, yaani Lumbila.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads