Magole
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Magole ni kata ya Wilaya ya Kilosa katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67414.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 11,752 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 20,954 [2] waishio humo.
Kijiji kimegawanyika katika yadi mbili, yaani Magole A na Magole B.
Magole A upande wa kushoto kuna vitongoji vya Manyata, Bwawani, Zizini, Kichangani.
Upande wa Magole B kuna vitongoji vya Mji Mkuu, Gendeni, Sinza na Chabwanga.
Shughuli kubwa za wakazi wengi ni kilimo cha biashara kama mahindi, mpunga, nyanya, mihogo, mtama na mazao mengine ya chakula
Mwaka 2014 kijiji kilikumbwa na mafuriko yaliyosababisha zaidi ya wakazi 500 kukosa nyumba.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads