Majoriko

From Wikipedia, the free encyclopedia

Majoriko
Remove ads

Majoriko (karne ya 5 - 484) alikuwa mtoto pekee wa Dionisya wa Vita; kwanza aliogopa dhuluma, lakini baadaye, kwa kufarijiwa na macho na maneno ya mama yake, akawa shujaa kuliko wenzake akafa katika mateso hayo.

Thumb
Mt. Dionisya na mwanae. Katika mchoro huo wa Jacques Callot (miaka ya 1630) mtoto Majoriko anahimizwa na mama yake Dionisya kuvumilia mateso ya kifodini.

Ni kati ya wafiadini wengi wa Kanisa Katoliki waliouawa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario.

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.[1]

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 6 Desemba.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads