Makambako
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Makambako ni mji na wilaya katika Mkoa wa Njombe, Tanzania, yenye postikodi namba 59113.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 146,481 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata 8 za Makambako zilikuwa na jumla ya wakazi 93,827[2] walioishi humo.
Hadi mwaka 2012 Makambako yenyewe ilikuwa kata ya Wilaya ya Njombe katika Mkoa wa Iringa. Kwa sasa ni mji wenye hadhi ya halmashauri ukiwa ni kitovu cha biashara mbalimbali na kilimo yakiwamo mazao ya mbao na nafaka.
Makambako ni njiapanda muhimu kusini mwa Tanzania. Barabara za TANZAM (Dar es Salaam - Mbeya) na barabara ya kuelekea Songea - Mtwara zinakutana huko, pamoja na kituo cha reli ya TAZARA.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads