Maksimo Muungamadini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Maksimo Muungamadini (Haspin, Siria, 580 hivi - Tsageri, leo nchini Georgia, 13 Agosti 662) alikuwa mmonaki padri maarufu kwa ari na teolojia yake.

Miaka 615-645 aliishi Karthago, leo nchini Tunisia.
Jina la pili aliongezewa kutokana na mateso yaliyompata kwa ajili ya imani sahihi dhidi ya waliokanusha utashi wa kiutu wa Yesu: chini ya kaisari Konstas II alikatwa mkono wa kulia na ulimi asiweze kuendelea kuitetea wala kwa maandishi wala kwa sauti.
Hatimaye alipelekwa uhamishoni pamoja na wanafunzi wake wawili wenye jina moja, Anastasi, na ndipo alipofariki[1].
Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli ulimpa ushindi baada ya kifo chake.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 13 Agosti[2] au 21 Januari.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads