Makumbusho ya Kitale

From Wikipedia, the free encyclopedia

Makumbusho ya Kitale
Remove ads

Makumbusho ya Kitale yanapatikana magharibi mwa Kenya, kilomita 380 kutoka mji mkuu wa Nairobi, na kilomita moja kutoka mjini Kitale.[1]. Ni makumbusho ya kwanza ya nyumbani nchini Kenya yaliyofunguliwa mwaka 1924.

Mwanzo makumbusho hayo yalikuwa yakijulikana kama The Stoneham Museum,[1] likiwa na jina la Colonel Hugh Stoneham aliyekuwa akikusanya vitu vya sanaa katika jumba hilo hadi alipofariki dunia mwaka 1966.

Baadaye mwaka 1974 makumbusho hayo yalifanywa kuwa makumbusho ya kitaifa na kuitwa Makumbusho ya Kitale.[2]

Thumb
Bango la makumbusho ya Kitale au Makumbusho ya Kenya magharibi.

Vitu vingi katika makumbusho hayo vimechukuliwa kutoka katika jamii za makabila mbalimbali ya Kenya, yakiwemo ya Waluyha, Wamaasai na Waturkana.[2] Makumbusho hayo yanaonyesha utamaduni halisi wa Wakenya, silaha walizotumia, vyombo vya kupikia, na ala za muziki.[2] Pia baadhi ya wanyama kama mamba, kobe na aina nyingi za nyoka hupatikana katika makumbusho hayo.[2]

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads