Malaika walinzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Malaika walinzi ni malaika wanaosadikiwa kuwa, mbali ya kutazama utukufu wa Mwenyezi Mungu, wametumwa naye kuongoza na kulinda binadamu mmojammoja au katika makundi madogo na makubwa katika safari ya maisha kwa uwepo wao ambao hauonekani lakini unawajibika [1][2]


Katika kalenda ya liturujia ya Kanisa la Kilatini, kumbukumbu yao inafanyika kila mwaka tarehe 2 Oktoba[3]. Kwa Waorthodoksi ni tarehe 11 Januari.
Remove ads
Historia ya imani hiyo
Imani hiyo ni ya zamani sana, ilijitokeza tayari katika Ugiriki wa Kale na katika Agano la Kale[4] na katika Agano Jipya[5], lakini ilistawishwa zaidi na Ukristo katika karne ya 5[6].
Imani ya namna hiyo katika Uislamu inapatikana katika Mu'aqqibat[7]
Sala kwa malaika mlinzi
Kwa Kilatini malaika mlinzi anaweza kuombwa hivi:
Angele Dei,
qui custos es mei,
me, tibi commissum pietate superna,
illumina, custodi,
rege et guberna.
Amen.[8]
Tafsiri yake ni:
Ee malaika wa Mungu,
uliye mlinzi wangu,
niliyewekwa kwako na huruma yake Mungu,
uniangaze, unilinde,
uniongoze, unitunze.
Amina.
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads