Malinyi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Malinyi ni kata ya Wilaya ya Malinyi katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67619.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 38,714 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 31,249 [2] walioishi humo.
Wakazi wa kata hii wanajishughulisha na kilimo cha mpunga. Mwaka 2012 shirika la umeme wa mwanga wa jua <TAREA> lilianza kusambaza umeme huo mji mzima.
Kuna shule za sekondari tano; shule hizo ni shule ya sekondari Malinyi, shule ya sekondari Kipingo, Shule ya sekondari Tira, shule ya sekondari Tumaini na shule ya sekondari Mtakatifu Pius.
Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika, kuna shule za msingi tano, nazo ni: shule ya msingi Nawigo, shule ya msingi Malinyi, shule ya msingi Makugira, shule ya msingi Makaerere na shule ya msingi Kipingo.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads