Wilaya ya Kinondoni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wilaya ya Kinondoni
Remove ads

Wilaya ya Kinondoni ni mojawapo ya wilaya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam yenye postikodi namba 14000. Kwa lugha nyingine ni manispaa ndani ya jiji la Dar Es Salaam.

Thumb
Mahali pa Kinondoni (kijani cheusi) katika mkoa wa Dar es Salaam.
Thumb
Picha ya angani ya Wilaya ya Kinondoni mnamo mwaka 2015.

Eneo lake ni sehemu za kaskazini za jiji. Kinondoni inaanza upande wa pwani kwenye Selander Bridge juu ya mto Upanga (pia: Msimbazi Creek) na kuendelea kupitia rasi ya Msasani, Kunduchi hadi Mbweni pamoja na hoteli za kitalii zilizopo sehemu hizo.

Barani inaelekea kuvukia barabara ya Morogoro hadi Mbezi na Kibamba. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo ndani ya manispaa hii.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Kinondoni ilihesabiwa kuwa 1,775,049 [1]. Baada ya wilaya kumegwa, katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 982,328 [2].

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads