Wilaya ya Ubungo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

(makala hii inahusu wilaya ya Ubungo, kuangalia makala ya kata ya Ubungo bonyeza hapa)

Ukweli wa haraka Nchi za, Mkoa ...

Wilaya ya Ubungo ni jina la mojawapo kati ya wilaya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 16000.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 1,086,912 [1].

Ubungo ilifahamika sana nchini kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani na miji mbalimbali ya Tanzania kama vile Arusha, Moshi, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Singida, Tanga na Mwanza; vilevile hadi Nairobi, Lilongwe, Lusaka na miji mingine kadhaa ya Afrika ya Mashariki.

Pia Ubungo ina barabara za juu na makao makuu ya Tanesco, shirika la umeme la Tanzania.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads