Mapatano ya Laterano

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mapatano ya Laterano
Remove ads

Mapatano ya Laterano kati ya Ufalme wa Italia na Ukulu mtakatifu yanaitwa hivyo kwa sababu yalisainiwa katika jumba la Laterano tarehe 11 Februari 1929.

Thumb
Ramani ya Mji wa Vatikani.

Lengo lake lilikuwa kumaliza suala la Roma lililovuruga Italia tangu mwaka 1870, nchi hiyo ilipoteka mji huo uliotawaliwa na Mapapa kwa karne nyingi.

Kwa mapatano hayo, Papa alikubali mji ubaki mikononi mwa Ufalme, isipokuwa mtaa wa Vatikano na majengo mengine machache. Ndivyo ilivyoundwa na kukubalika kimataifa nchi huru ya Mji wa Vatikani iliyomwezesha Papa kuwa huru katika kuongoza Kanisa Katoliki duniani kote.

Mapatano hayo yaliheshimika hata baada ya serikali ya Ufashisti kuanguka, Italia kugeuka Jamhuri na katiba mpya kutungwa. Tena hiyo ilijumlisha mapatano hayo ndani yake[1].

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads