Mashahidi wa Yehova

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mashahidi wa Yehova
Remove ads

Mashahidi wa Yehova (kwa Kiingereza Jehovah's Witnesses) ni wafuasi wa dini jamii ya Ukristo ambayo ilianzia Marekani na kuenea ulimwenguni kote.

Thumb
Makao makuu ya kimataifa huko Brooklyn, New York, Marekani.

Tofauti na Wakristo karibu wote, hao hawamuamini Yesu kuwa Mungu sawa na Baba, wala Roho Mtakatifu kuwa nafsi, na kwa jumla hawakubali imani katika Utatu wa nafsi katika Mungu pekee. Kwa sababu hiyo madhehebu mengi hayawatambui kama Wakristo wala hayakubali ubatizo wao.

Mwanzilishi alikuwa Charles Taze Russell pamoja na kikundi cha wanafunzi wa Biblia (miaka ya 1870). Jina la sasa lilianza kutumika mwaka 1931.

Kwa sasa wako milioni 8.7 katika jumuia 120,387.[1]

Kwa sababu hizo katika nchi mbalimbali dini hiyo iliwahi kukatazwa, kama nchini Tanzania wakati wa urais wa Julius Nyerere au bado ni marufuku.

Remove ads

Hoja dhidi yao

Wengi wamelaumu Mashahidi wa Yehova hasa kutokana na jinsi walivyotafsiri na wanavyofafanua Biblia, mafundisho yao, katazo la utoaji damu, kutokubali matibabu yanayohusisha damu, mara kadhaa za utabiri wao kutotimia hasa kuhusu mambo ya mwisho, pamoja na jinsi waumini wanavyofuatiliwa na kushinikizwa na viongozi wao.

Kwa sababu hizo na kwa kutokubali kwa sababu ya dhamiri kujiunga na jeshi, kusalimu bendera za taifa au kuimba nyimbo za Taifa , pamoja na msimamo wao wa kutounga mkono upande wowote katika siasa, katika nchi mbalimbali dini hiyo iliwahi kukatazwa, kama nchini Tanzania wakati wa urais wa Julius Nyerere au bado ni marufuku kama vile huko Kazakstan, Eritrea na sasa Urusi.

Wenyewe wamekataa daima lawama hizo, lakini kila mwaka wengi wanajitenga nao.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads