Mathayo Alonzo Leciniana

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mathayo Alonzo Leciniana
Remove ads

Mathayo Alonzo Leciniana, O.P. (1702-1745) alikuwa padri Mdominiko wa Hispania.

Thumb
Mt. Mathayo Alonzo alivyochorwa.

Baada ya kuhubiri Injili bila kujibakiza nchini Vietnam, hata akiwa kifungoni, aliuawa kwa kuchomwa kwa upanga pamoja na Fransisko Gil de Frederich [1].

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, ila ya kwake mwenyewe ni tarehe 22 Januari[2][3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads