Mathayo Gam Van Le
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mathayo Gam Van Le (1813 - 1847) alikuwa Mkristo wa Vietnam aliyekatwa kichwa kwa amri ya kaisari Thieu Tri baada ya kukaa gerezani mwaka mzima kwa sababu aliingiza nchini kwa boti lake wamisionari kutoka Ulaya [1].

Ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886). Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 11 Mei[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads