Matilda wa Ringelheim
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Matilda wa Ringelheim (kwa Kijerumani Mathilde von Ringelheim; 894/897 – 14 Machi 968) alikuwa malkia mdogo wa Saxony kuanzia mwaka 912 na malkia wa Ujerumani mzima kuanzia mwaka 919 kutokana na ndoa yake na Henry I, mfalme wa kwanza wa nasaba ya Otto.

Mke mwaminifu kabisa, alikuwa na unyenyekevu na subira sana; pia alijitahidi kusaidia watu fukara na kujenga hospitali na monasteri [1].
Baada ya kufiwa mumewe mwaka 936, alianzisha abasia ya Quedlinburg kwa heshima yake. Matilda aliishi hadi kuona Dola la Roma la Magharibi kuanzishwa tena na mwanae wa kwanza, Otto I aliyetiwa taji mwaka 962.
Baada ya hapo alikwenda kutawa katika abasia hiyo ambapo ndipo alipofariki.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake, 14 Machi[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads