Popo-wadudu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Popo-wadudu
Remove ads

Popo-wadudu ni aina za popo wanaowinda wadudu hasa. Kibiolojia ni mamalia wa nusuoda Yangochiroptera katika oda Chiroptera wanaofanana na panya wenye mabawa. Kwa kawaida spishi hizi ni ndogo kuliko zile za nusuoda Yinpterochiroptera (popo-matunda) lakini kuna spishi zilizo kubwa kulika spishi fulani za popo-matunda. Spishi ndogo kabisa ni popo nyukibambi aliye na urefu wa mm 29-33 na uzito wa g 2. Kwa hivyo popo huyu ni spishi ndogo kabisa ya mamalia pia. Kirukanjia wa Etruski anaweza kuwa na uzito mdogo zaidi (g 1.2-2.7) lakini ni mrefu zaidi (mm 36-53). Popo-wadudu hula wadudu hasa lakini spishi nyingine hula samaki, ndege na wanyama wadogo na hata damu. Hutumia miwangwi ya sauti yao ili kuyakamata mawindo yao. Spishi kadhaa hula matunda na mbochi na hizi hazitumii miwangwi.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Mwainisho[1]

Oda: Chiroptera

  • Nusuoda Yangochiroptera
    • Familia Cistugidae (Popo mabawa-tezi)
    • Familia Emballonuridae (Popo mkia-uo)
    • Familia Furipteridae (Popo bila gumba)
    • Familia Miniopteridae (Popo mabawa-marefu)
    • Familia Molossidae (Popo mkia-huru)
    • Familia Mormoopidae (Popo uso-pepo)
    • Familia Mystacinidae (Popo mkia-mfupi wa Nyuzilande)
    • Familia Myzopodidae (Popo miguu-minaso)
    • Familia Natalidae (Popo masikio-mpare)
    • Familia Noctilionidae (Popo wavuvi)
    • Familia Nycteridae (Popo uso-kibonde)
    • Familia Phyllostomidae (Popo pua-jani)
    • Familia Thyropteridae (Popo mabawa-minaso)
    • Familia Vespertilionidae (Popo-jioni)
Remove ads

Picha

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads