Mkunga Mfyonzaji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mikunga wafyonzaji ni wanyama wa oda Petromyzontiformes katika ngeli Hyperoartia wanaofanana na mikunga wa kawaida lakini ni wanyama tofauti sana. Wao ni ukoo wa kale wa samaki bila mataya. Mkunga mfyonzaji aliyekomaa anaweza kuainishwa kwa kuwa na kinywa cha kufyonzia kwa umbo wa mpare kilicho na meno makali. Pamoja na mikunga-ute (ngeli Myxini) wanaunda ngeli ya juu Cyclostomata (maana: wenye kinywa cha mviringo).

Kuna spishi 18 za mikunga wafyonzaji zilizopo. Spishi hizi ni vidusia waladamu na hula kwa kuchochea ndani ya mwili wa samaki wengine ili kufyonza damu yao[1]. Spishi 9 baina hizi huhamia kutoka kwa maji ya chumvi hadi maji baridi ili kuzaliana (baadhi yao pia wana idadi za maji baridi) na tisa wanaishi katika maji baridi tu. Katika ngeli Hyperoartia kuna spishi 20 nyingine zisizofyonza damu na hizi ni spishi za maji baridi[2]. Waliokomaa wa spishi hizi hawali; wanaishi wakila akiba waliyopata kwa njia ya kuchuja chakula kutoka maji wakati walikuwapo lava au amoseti (Kiing. ammocoetes).
Remove ads
Msambazo
Mikunga wafyonzaji huishi zaidi katika maji ya pwani, ingawa spishi kadhaa (k.m. Geotria australis, Petromyzon marinus na Entosphenus tridentatus) husafiri umbali mkubwa kiasi katika bahari wazi[3] kama inavyothibitishwa na ukosefu wao wa kutengwa kwa uzazi kati ya idadi. Spishi kadhaa hupatikana katika maziwa yaliyozungukwa kwa ardhi. Hupatikana katika maeneo mengi ya wastani lakini hawatokei katika Afrika. Lava zao (amoseti) zina uvumilivu mdogo kwa maji ya joto kiasi, ambalo linaweza kueleza kwa nini hawasambawi katika kanda za tropiki.
Remove ads
Mofolojia
Waliokomaa hufanana kijuujuu na mikunga kwa kuwa wana mwili mrefu bila magamba na huweza kuwa na urefu wa sm 13-100. Mikunga wafyonzaji waliokomaa wana macho makubwa, tundu moja la pua juu ya kichwa na matundu saba ya matamvua kila upande wa kichwa, lakini wanakosa jozi za mapezi. Koromeo limegawanyika, sehemu ya chini ikiunda neli ya kupumua ambayo imetengewa kinywa kwa vali inayoitwa velo ([[Kiing. velum).
Tabia za kipekee za kimofolojia za mikunga wafyonzaji, kama vile kiunzo chao cha gegedu, huonyesha kuwa ni kundi la dada la vertebrata wote walio na mataya (Gnathostomata). Mara nyingi huchukuliwa kama kundi la msingi la vertebrata[4] . Badala ya pingili za uti wa mgongo za kweli wana mfululizo wa miundo ya gegedu inayoitwa arkualio iliyopangwa hapo juu ya ugwe wa neva.
Remove ads
Picha
- Geotriidae (Geotria australis)
- Mordaciidae (Mordacia lapicida)
- Petromyzontidae (Lampetra fluviatilis)
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads