Etna

From Wikipedia, the free encyclopedia

Etna
Remove ads

Etna (kutoka Kilatini: Aetna; kwa Kiitalia pia Mongibello; kwa Kisisili Mungibeddu au â Muntagna) ni volkeno hai wa Sicilia mashariki (Italia visiwani) kati ya miji ya Catania na Messina. Ndiyo ndefu kuliko zote za Ulaya[1]: kwa sasa imefikia mita 3357 juu ya usawa wa bahari.[2]

Thumb
Etna ikiwa na Catania chini yake.
Thumb
Etna nyuma ya milima Peloritani.
Thumb
Hoteli Sapienza, inayofikiwa na watalii wengi.
Thumb
Theluji inatumika kwa mchezo wa skii.

Etna inaenea katika kilometa mraba 1190 ukiwa na duara ya km 140 miguuni pake. [3]

Etna inakadiriwa kuwa na miaka 350,000 - 500,000 na ni kati ya volkeno hai zaidi duniani, kwa kuwa haitulii karibu kamwe, lakini kwa namna yake si hatari. Lava yake inageuka baada ya miaka kadhaa kuwa nzuri sana kwa kilimo.

Mnamo Juni 2013 iliingizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.[4]

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads