Mnandi-pwani

Jenasi ya ndege wa bahari From Wikipedia, the free encyclopedia

Mnandi-pwani
Remove ads

Minandi-pwani ni ndege wa bahari wa jenasi Fregata, jenasi pekee ya familia Fregatidae. Wana domo refu lenye ncha kwa kulabu, mabawa marefu na mkia wenye panda. Rangi yao ni nyeusi; jike ana tumbo jeupe na dume ana mfuko wa koo mwekundu ambao anaweza kumvimbisha ili kumvutia jike. Ndege hawa hawaogelei na watembea kwa shida, kwa hivyo wako hewani takriban saa zote. Wanaweza kukaa hewani hata zaidi ya wiki moja. Kama shakwe-waporaji, huonekana mara nyingi wakipora mateka kwa ndege wengine, lakini chakula chao hasa ni samaki, ambao huwakamata wakiruka, na kwa kiasi kidogo zaidi makinda ya ndege. Jike hutaga yai moja au mayai mawili juu ya mti au ardhini au juu ya mwamba wa pwani.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi ya bara jingine

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads