Mnazi (mti)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mnazi (mti)
Remove ads

Mnazi (Cocos nucifera) ni kati ya miti muhimu zaidi kwa ajili ya uchumi wa kibinadamu katika nchi za tropiki.

  • tunda lake laitwa nazi ni chakula
  • nyama ya tunda hukaushwa kuwa nguta (au: mbata). Nguta hutumiwa viwandani kwa kutengeneza mafuta ya kulika.
  • utomvu ni kinywaji chenye afya kwa sababu ya vitamini yake
  • utomvu uliochachuka "mnazi" ni kinywaji cha pombe
  • ubao unatumiwa kwa ujenzi wa nyumba au jahazi
  • majani kwa paa za nyumba, mikeka au makofia.
  • Mafuu ya mbegu hutumiwa kama kuni au kutengeneza vifaa vya muziki au urembo kama vile bandili, hereni au mikufu.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...

Mnazi ni mmea wa familia ya Palmae (au: Arecaceae). Asili yake inafikiriwa iko Asia ya kusini lakini umesambaa tangu karne nyingi sana. Mbegu wake unaweza kuzaa hata baada ya kukaa kwenye maji ya bahari kwa muda fulani hivyo inawezekana ya kwamba mnazi ulisambaa peke yake kwenye pwani za bahari. Lakini bila shaka watu waliibeba safarini kwa sababu ni chakula.


Remove ads

Viungo vya Nje

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads