Msongola

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Msongola ni moja ya kata (ward) ya Wilaya ya Ilala katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 12114. Kata hiyo imepakana na Mbande ambayo ipo wilaya ya Temeke, imepakana pia na mkoa wa Pwani, imepakana pia na Kitunda Kivule na Chanika ambazo zipo wilaya ya Ilala.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 94,923 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Msongola ilikuwa na jumla ya watu 46,989, wakiwemo wanawake 24,584 na wanaume 22,401 katika kaya zaidi ya 10,418.[2][3]

Msongola ina vitongoji vitano ambavyo ni: Yangeyange, Mbondole, Mvuleni, Kitonga na Mvuti.

Msongola ina zahanati za serikali tatu ambazo ziko Mvuti, Kitonga na Msongola.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads