Benue (mto)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Benue (mto)
Remove ads

Mto Benue (kwa Kifaransa: Bénoué) ni tawimto kubwa la mto Niger. Chanzo chake ni katika nyanda za juu za Kamerun, hasa milima ya Adamawa.

Ukweli wa haraka Mto wa Benue ...

Katika sehemu ya kwanza ya mwendo wake unatelemka mita 600 kwa mwendo kali. Karibu na mji wa Garua unaungana na mto Mayo Kébi. Baada ya mwendo wa km 350 mto huo unatoka Kamerun na kuingia Nigeria karibu na bandari ya Jimeta. Huko mto una upana wa kilomita moja unaoweza kupanua wakati wa mvua. Baada ya Yola mto unapokea tawimto lake muhimu zaidi, mto Gongola.

Katika Nigeria mto ni njia muhimu ya kusafirisha mizigo na mazao ya nchi kati ya pwani ya Atlantiki na sehemu za bara.

Unaishia katika mto Niger kwenye mji wa Lokoja.

Remove ads

Tazama pia

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Benue (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads