Mto Marne

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mto Marnemap
Remove ads

Marne ni mto wa Ufaransa, tawimto upande wa kulia wa Seine katika eneo la mashariki na kusini ya Paris. Una urefu wa kilometre 514 (mi 319).[1] Mto ulizipatia jina lake wilaya za Haute-Marne, Marne, Seine-et-Marne, na Val-de-Marne.

Thumb
Kisiwa katika mto Marne karibu na Chelles
Ukweli wa haraka Marne ...

Mto Marne unaanza katika platuu ya Langres, unatiririka kuelekea kaskazini, kisha unaelekea magharibi kati ya Saint-Dizier na Châlons-en-Champagne, na kuungana na Seine katika Charenton katika Paris. Katika kanda la Champagne sehemu ya maji huongozwa katika ziwa la kujengwa na binadamu la Lac du Der-Chantecoq, ili kudhibiti mtiririko wa maji. Kwa njia hiyo kiwango cha maji cha chini huzuiwa.[2]

Mto Marne ulikuwa eneo la mapigano mawili wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. La kwanza Lilikuwa mgeuko wa Vita vya Kwanza vya Dunia katika mwaka wa 1914. La pili lilitokea miaka minne baadaye, katika mwaka wa 1918.

Thumb

Katika karne ya 19 na 20, Marne ulipendeza wachoraji na wasanii wengi; miongoni mwao ni:

  • Camille Corot
  • Paulo Cézanne
  • Camille Pissarro
  • Henri Rousseau, dit "Le Douanier Rousseau"
  • Albert Marquet
  • Raoul Dufy
  • André Dunoyer de Ségonzac
  • [Louis Vuillermoz]
  • Maurice Boitel
  • Daniel du Janerand
Remove ads

Wilaya na miji iliyopitwa na mto huu

Thumb
Ufuko wa Marne katika Noisy-le-Grand


Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads