Shebeli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Shebeli (pia: Shabelle, Scebelli, Shabell, Shebele) ni tawimto la mto Juba linalobeba maji yake kutoka nyanda za juu za Ethiopia kuelekea Bahari ya Uhindi ingawa mara nyingi inakauka katika jangwa la Somalia kabla ya kufikia mdomo wake.

Chanzo cha Shebeli kiko katika milima ya Batu (Ethiopia) takriban km 200 kusini kwa Addis Ababa.
Baada ya mwendo wa km 920 mto unaingia Somalia ikielekea Mogadishu. Karibu na mji unageukia kusini-magharibi na kufuata mstari wa pwani ya Bahari Hindi kwa umbali wa km 20-40 ndani ya bara.
Baada ya mwendo wa km 900 ndani ya Somalia lalio lake linaingia katika mto Juba lakini baada ya Mogadishu Shebeli ni kavu kwa sehemu kubwa ya mwaka.
Remove ads
Tazama pia
- Mito mirefu ya Afrika
- Orodha ya mito ya Ethiopia
- Orodha ya mito ya Somalia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads