Mto Songhua
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mto Songhua (kwa Kirusi: Сунгари, Sungari) ni kati ya mito mikubwa nchini China, pia ni tawimto kubwa la Amur. Songhua ina njia ya km 1,927 kutoka Milima ya Changbai iliyopo kwenye mpaka wa China na Korea Kaskazini kupitia mikoa wa kaskazini ya China.

Mto huo una beseni la km2 557,180[1] [2] ukibeba m³ 2,463 za maji kila sekunde.[3]
Songhua inapita katika tambarare ya China kaskazini iliyo na mtelemko mdogo sana na hivyo njia ya mto ni ya kupindapinda ukiacha mahali penye maziwa madogo kama mabaki ya njia zake za awali.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads