Mto Songwe (Songwe)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kwa mto mwingine wenye jina hili, tazama Songwe (Mbeya).
Mto Songwe (au Songwe ya Kaskazini) ni kati ya mito ya mkoa wa Songwe (Tanzania Kusini Magharibi). Mto huo, ambao umeupa mkoa jina lake, una chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya iliyopo kusini ya Mbeya ikielekea kaskazini na kuishia Ziwa Rukwa.
Bonde lake limejulikana kati ya wataalamu wa akiolojia kwa mifupa na mabaki ya nyakati za kale zinazopatikana hapa.
Barabara ya Mbeya kwenda Zambia inavuka mto Songwe penye kiwanda cha saruji inayotumia mawe ya bonde la mto.
Mto unapita baadaye karibu na kijiji cha Galula kabla ya kufikia ziwa Rukwa.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads