Mto Turkwel

ni mto unaotoka mlima Elgon mpakani mwa Kenya na Uganda hadi Ziwa Turkana. Mto huu unaitwa Mto Suam kutoka chanzo chake hadi mpakani katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya. From Wikipedia, the free encyclopedia

Mto Turkwel
Remove ads

Mto Turkwel[1] (pia: Turkwell[2][3]) unapatikana katika kaunti ya Turkana nchini Kenya na unaishia katika ziwa Turkana, lililo kubwa kuliko maziwa yote ya jangwani yaliyoko duniani kote[4].

Thumb
Mto Turkwel ukiwa umekauka karibu na Lodwar.

Chanzo chake ni katika Mlima Elgon, mpakani mwa Kenya na Uganda na unaitwa kwanza mto Suam. Upande wa kaskazini wa Kapenguria katika kaunti ya West Pokot njia yake imezuiwa na lambo linalounda Bwawa la Turkwel.

Mara nyingi maji yake hayatoshi kufika ziwani na mto unakauka mapema.

Delta ya mto Turkwel Delta inapatikana kwenye mita 369 juu ya usawa wa bahari, mara baada ya kuingia katika kaunti ya Marsabit[5]. 3°06′17″N 36°05′51″E

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads