Lambo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Lambo
Remove ads

Lambo ni ukuta uliojengwa kwa kusudi la kuzuia mwendo wa maji au kubana maji katika eneo fulani. Mara nyingi malambo hujengwa kufunga njia ya maji ya mto. Lambo laweza pia kukusanya maji ya mvua kwenye njia ya mtelemko wake.

Thumb
Lambo la Aswan kwenye Ziwa la Nasser katika Misri
Thumb
Ukuta wa lambo

Shabaha ya kujenga lambo

Shabaha ya kujenga lambo ni hasa kupata akiba ya maji. Maji hutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji, kama chanzo cha maji ya bomba kwa ajili ya watu au pia kwa utengenezaji wa umememaji.

Lambo hujengwa pia kwa shabaha ya kuzuia mafuriko.

Malambo hujengwa mara nyingi katika mabonde ambako milima ya pande zote mbili iko karibu na kupunguza mahitaji ya kujenga ukuta mkubwa mno.

Kuna pia malambo ya bahari ambayo yanajengwa kama hifadhi ya nyumba au mashamba dhidi ya maji ya bahari.

Remove ads

Shida za malambo

Kuna pia matatizo ya malambo:

  • Ukuta unaathiri uwiano wa ekolojia; kwa mfano lambo la Aswan linazuia matope yenye rutuba yasifikie Misri
  • Umwagiliaji katika nchi za joto unaweza kuharibu ardhi ukiiongezea chumvi kwa njia ya uvukizaji
  • Mara nyingi wenyeji wamefukuzwa katika eneo la ziwa jipya bila kupewa makazi mazuri
  • Penye hatari ya tetemeko la ardhi uzani wa maji umeongeza matetemeko
  • Lambo linaweza kusababisha ajali na hata maafa likipasuka na kiasi kikubwa cha maji kilichozuiliwa na ukuta wake kushuka ghafla na kuharibu makazi ya watu, mashamba na miundombinu kwenye njia yake[1].
Remove ads

Malambo makubwa ya Afrika

Picha za malambo

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads