Mwana FA

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Hamis Mohammed Mwinjuma, anayejulikana pia kama Mwana FA[1] ni mwanamuziki, mjumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), na mwanasiasa[2] anayehudumu kama Mbunge wa jimbo la Muheza tangu Novemba 2020. Anajulikana kwa nyimbo zake kama Endelea Tu na Unanijua Unainiskia[3].

Ukweli wa haraka Jina la kuzaliwa, Amezaliwa ...
Remove ads

Wasifu

Hamis Mwinjuma alizaliwa Muheza, Tanga, Tanzania. Mwaka 2016 alifunga ndoa na Bi Helga Mwinjuma wakafanikiwa kupata watoto wawili. Mwinjuma na familia yake wanaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania[4].

Elimu

Mwana Fa alianza elimu yake ya msingi katika shule ya msingi ya Mdote huko Muheza.[5]. Alijiunga na chuo cha Dar es salaam Institute of Technology kwa ajili ya masomo yangazi ya juu. Hata hivyo alikatiza masomo yake miezi minne tu baada ya udahili ili kujiunga na elimu ya upili katika shule ya sekondari ya Ununio Islamic akienda na mchepuo wa fizikia, kemia na hisabati[6]. Alifanya stashahada ya Juu ya uchumi kwa mwaka mmoja katika taasisi ya fedha. Baadaye alifanikiwa kufanya Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Fedha kutoka katika taasisi hiyo hiyo. Mwinjuma alihitimu taaluma ya Usimamizi wa uchumi mwaka 2007, pia ana cheti cha teknolojia ya habari na shahada ya uzamili ya fedha kutoka Coventry, Uingereza.

Remove ads

Shughuli za Muziki

Mapenzi yake na muziki yalianza kuonekana tangu akiwa na umri mdogo wa miaka kumi na miwili. Alianza kuimba akiwa shule ya msingi. Mwana Fa aliunda kundi lake la kwanza, lililoitwa Black Skin hiyo ilikua mwaka 1995 ambalo lilikuwa na wanafunzi wenzake Robby Ras na Generics. Kundi hilo liliibuka katika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Hip Hop ya Tanga mwaka mmoja baadaye. Kwa bahati mbaya kundi hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani wanachama walikuwa na njia tofauti katika maendeleo kitaaluma. Hata hivyo, Mwinjuma aliendelea kunoa kipaji chake akiwa katika shule ya upili na kuanza kutoa vibao bora zaidi happ baadaye[7].

Mbali na siasa Mwana Fa ni mfanyabiashara na mjasiriamali, pia amekuwa balonzi wa makampuni mbali mbali hapa Tanzania.

Shughuli za siasa

Mwaka 2020, Mwinjuma alijiunga na ulingo wa siasa nchini Tanzania alipowania kiti cha ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akishinda dhidi ya Yosepher Komba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kupata kura 47,578 za ubunge wa Jimbo la Muheza. Pia Mwana FA ni naibu waziri wa sanaa na michezo Tanzania.[8].

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads